• Seynation Updates

    Tuesday, 12 June 2018

    Rosa Ree Afichua Tetesi Zilizokuwepo Kuhusu Kujiunga WCB



    Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Rosa Ree amejibu iwapo alishafanya mazungumzo na WCB kwa lengo la kujiunga na label hiyo.

    Rosa Ree ambaye awali kabisa alikuwa katika label ya The Industry ameiambia Bongo5 kuwa hawajawahi kuzungumza hilo ila ni watu ambao wamekuwa bega kwa bega na yeye katika muziki wake.

    “Hapana ilikuwa hamna, ndiyo timu mzima ya WCB wamekuwa wakinisapoti katika muziki wangu. Nafurahia hilo ila hatukuwahi kufikia hatua hiyo,”

    Utakumbuka October 2017 wakati Rosa Ree anaweka wazi kumalizika kwa mkataba wake The Industry katika mahojiano na Bongo5 alijibu kuhusu hilo pia.

    “Am open to anything as long as ina manufaa kwangu but hatujaongea” alisema.

    Rosa Ree kwa sasa yupo katika label ya Dimo Production kutoka nchini Afrika kusini ambayo ndio imefanikisha kolabo yake ‘ Way Up’ na rapper Emtee kutoka nchini Afrika Kusini.




    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI