Manchester United watakutana na klabu ya Wolfsburg kutoka Ujerumani
Michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne Desemba 8 kwa michezo kadhaa katika hatua ya makundi.
Real Madrid itakuwa ikichuana dhidi ya Malmo, Paris Saint-Germain watawakabili Shakhtar Donetsk zikiwa ni mechi za kundi A.
KUNDI: B:
PSV Eindhoven Wao watapepetana na CSKA Moskva, Wolfsburg watakuwa wakimenyana na Manchester United .
KUNDI: C:
Benfica watawakabili Atlético Madrid, na Galatasaray ya Uturuki itachuana na Astana
KUNDI: D:
Manchester City Watawakabili Borussia Mönchengladbach, huku Sevilla wao wakichuana na vijukuu vya bibi kizee vya Turin Klabu ya Juventus .
Na Desemba 9 kutapigwa mechi kadhaa katika mwendelezo wa michuano hiyo.
Monday, 7 December 2015
Home
Unlabelled
Man Utd kukabiliana na Wolfsburg UEFA
No comments:
Post a Comment