• Seynation Updates

    Friday, 24 June 2016

    MCHEZAJI APEWA KADI NYEKUNDU KISA KUTOA HEWA CHAFU UWANJANI

    Katika soka kuna mengi ya kuchekesha lakini hili la muamuzi wa Sweden linaweza likawa la kushangaza zaidi, refa mmoja raia wa Sweden amefanya maamuzi ambayo yamewashangaza wengi, kufuatia uamuzi wake wa kumuonesha kadi mbili za njano mchezaji Adam Lindin.
    Refa aliamua kumuonesha kadi ya kwanza ya njano Adam Lindin baada ya kutoa hewa chafu mbele yake, baada ya mchezaji huyo kushangaa kwa kuoneshwa kadi ya njano, refa alimuonesha kadi ya pili ya njano iliyopelekea mchezaji huyo kutoka nje ya uwanja, refa alifanya maamuzi hayo akiamini tukio hilo la Adam sio la kiuchezaji.
    160624103052_adam_lindin_512x288_bbc_nocredit
    Adam Lindin
    Tukio la refa kumuonesha mchezaji kadi nyekundu kwa kutoa ushuzi uwanjani limetajwa kuwa ndio la kwanza katika, kiasi ambacho kimepelekea gumzo kubwa mitandaoni, Adam Lindin mwenye miaka 25 ni nyota wa klabu ya  Pershagen SK inayoshika mkia katika Ligi KuuSweden.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI