Kwa muda mrefu Wakenya walikuwa wakidai kutozielewa nyimbo za Victoria Kimani na yeye mwenyewe mara kibao amewahi kulalamika kutopewa support ya kutosha nchini mwao.
Na sasa muimbaji huyo mrembo huenda akawa amepata dawa ya tatizo hilo. Kimani ameachia single ya kwanza ya Kiswahili iitwayo ‘Gota.’
Kimani amemtaja rapper,Abbasdoobeez kuwa ndiye aliyemsaidia kuandika wimbo huo kwa Kiswahili. Wimbo huo uliotambulishwa jana kupitia Kiss FM ya Kenya, bado haujawekwa mtandaoni.
“ASANTE SANA !!! Thank you so much for Tuning in!!!!! Gawdddd I’ve never been so nervous Online Link will be out in a few #GOTA,” aliandika kwenye Twitter.
No comments:
Post a Comment