• Seynation Updates

    Monday 19 September 2016

    Linex Kufanya Collabo Na Jose Chameleone



    Msanii wa muziki nchini, Linex Sunday Mjeda ameweka wazi mpango wake wa kufanya kolabo na staa wa muziki kutoka nchini Uganda, Dr. Jose Chameleone. Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Linex amesema tayari ameshamtumia Jose beat kwa ajili ya maandalizi ya wimbo huo mpya.
    “Mimi kwa upande wangu nimeshaingiza verse, bado Jose lakini na yeye aliniambia ataingiza Jumatatu hii kwa sababu nilishamtua beat,” alisema Linex. “Kwa hiyo ni kazi ambao itakuja ikikamilika lakini siyo soon, kwa sababu kuna mambo mengi yanakuja kutoka kwangu hivi karibuni,”
    Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wake kuendelea kusubiria video ya wimbo ‘Hewala’ aliomshirikisha mkali wa masauti Christian Bella.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI