Kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amesema kuwa Tottenham inaweza kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza baada ya ku stopisha ushindi wa mechi 13 mfululizo wa Chelsea kwa kuifunga 2-0 katika uwanja wa White Hart Lane.
Magoli mawili ya vichwa vilivyopigwa na Dele Ali viliisaidia Tottenham kuishinda Chelsea tangu mwezi Septemba na kuiacha Spurs ikiwa pointi saba nyuma ya viongozi hao katika nafasi ya tatu.
”Tottenham ni timu nzuri sana na kwa kweli ni mojawapo ya timu ambazo zinaweza kuwania taji la ligi”, alisema Conte baada ya mechi hiyo.
Kocha Mauricio Pochettino alisema kuwa Spurs inaweza kupigania vitu vikubwa.
Msimu huu hawajafungwa nyumbani katika ligi na Pochettino ,mwenye umri wa miaka 44 anasema kuwa matokeo mazuri ndio yatakayosaidia kupanda katika kilele cha ligi.
Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye FACEBOOK na INSTAGRAM @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.
No comments:
Post a Comment