Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwakamata wamiliki wapikipiki ambao watashindwa kuwa na kofia ngumu za pikipiki maarufu kama bodaboda.
Waziri Mwigulu ameyaongea hayo akiongea na madareva wa pikipiki wa wilaya ya shinyanga ambao wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani mkoani humo, Waziri Mwigulu amesema Polisi sasa wakiwakamata madereva wa pikipiki wakiwa hawana kofia ngumu wawaulize mmiliki wa pikipiki ni nani naye akamatwe aulizwe kwanini hana kafia ngumu awekwe ndani
Waziri Mwigulu amesema pia kama abiria naye akikataa kuvaa kofia ngumu na wakati pikipiki ina kofia hizo basi naye akamatwe na dereva pikipiki achiwe aendelee na biashara kwani kila mtu lazima atimize wajibu wake hivyo anatoa mwezi mmoja madereva wote wa pikipiki na wamiliki wahakikishe wanakofia ngumu mbili za pikipiki.
Naye mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Steven Masele amesema zamani palikuwa na msugaono mkubwa sana kati ya madereva wa pikipiki na askari wa jeshi la polisi hali iliyopelekea kutokuwa na mahusiano mazuri kati yao lakini kwasasa hivi kuna uhusiano mzuri uliojengwa na RPC mpya.
Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga ACP Simon Haule amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa maagizo na mkuu wamkoa baada ya wananchi wengi kutojua au kutokutumia sheria ya matumizi ya barabara hasa katika mzunguko (roundabout).
Naye mmoja wa madereva wa pikipiki wilaya ya shinyanga ameeleza kwasasa changamoto kubwa wanayokutana ni mfumo usiorafiki wa upatika wa leseni ya udereva hivyo kufanya madereva wengi wapikipiki kutokuwa na leseni kwani ni zaidi ya miezi sita tangu alipie kupata leseni hiyo. Waziri Mwigulu amesema anachukua hilo watalifanyia kazi.