ZIKIWA zimepita siku chache tangu kuachiwa mtandaoni picha zinazomuonesha msanii wa Bongo Fleva na muuza nyago, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ akiwa nusu utupu na Mbongo Fleva, David Genzi ‘Young D’, ishu hiyo imetinga ndani ya Baraza la Sanaa Taifa (Basata).
Akizungumza Katibu wa Baraza la Sanaa Taifa (Basata), Godfey Mwingereza amesema kuwa malalamiko na picha hizo zimewafikia na wapo katika hatua ya kuwafanyia uchunguzi wa kina kabla ya kulitolea tamko.
“Suala hili limetufikia lakini bado ni mapema kutoa maamuzi mpaka ufanyike uchunguzi, ingekuwa mazingira yake yanaonyesha kwamba wapo kwenye shughuli za muziki hapo ningekuwa na majibu ya haraka maana sisi tunaangalia masuala ya kazi si mambo binafsi ya msanii,”