Meli hiyo inayofanya shughuli zake za usafirishaji kati ya Mwanza na kisiwa cha Gozba Wilayani Muleba Mkoani Kagera, ilizama majira ya saa nne usiku ikiwa na nahodha, wabeba mizigo pamoja na mzigo wa magunia 750 ya dagaa.
Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kubaini kama kuna waliosahaulika majini, na taarifa zaidi zitatolewa baada ya zoezi hilo kukamilika.Watu 17 wameokolewa baada ya meli ya MV Julius kuzama ziwa Victoria jana usiku ikiwa na watu pamoja na mizigo, kilomita chache kutoka kisiwa cha Goziba Wilayani Muleba Mkoani Kagera.