Tatizo la msongamano katika hospitali za rufaa limekuwa ni jambo la kawaida kutokana na hospitali nyingi kukosa huduma ya chakula kwa wagonjwa, hivyo ndugu na jamaa wa wagonjwa hutumia fursa hiyo kupeleka chakula hospitalini jambo ambalo huonekana kuwa kikwazo kwa wauguzi hasa wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kutokana na kukithiri kwa kero hiyo ya mwingiliano wa majukumu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi mwaka huu, ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa hospitalini hapo na kupunguza msongamano muda wa kazi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa
huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa ambapo amebainisha kuwa muda uliowekwa awali kwa ajili ya chakula hautokuwepo.
“Aidha hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo muda wa kuona wagonjwa sasa utakuwa saa 12 asubuhi hadi saa 1 na jioni saa 10 jioni ule muda wa saa 6-8 mchana hautokuwepo tena”. Alisema Aligaesha
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sister Agness Mtawa amesema katika kuanzisha huduma hiyo wamezingatia wagonjwa wa makundi maalum kuhusiana na vyakula vyao.
“Tumezingatia wenye kisukari, presha na kifua kikuu kutakuwa na uangalizi maalumu maana kuna watu walisahau majukumu yao kutokana na mgonjwa mmoja kuja kutazamwa na ndugu saba wanajikuta wanatekeleza majukumu yaliyotakiwa kufanywa na wahudumu wa afya sasa tunarudi kazini wasioweza kula wenyewe watalishwa na wauguzi ni wajibu wetu”. Alisema Sister Mtawa.
No comments:
Post a Comment