Rapa Roma Mkatoliki amedai japo matatizo aliyoyapata yalikuwa makubwa lakini hawezi kueleza yatakuwa yamemuathiri kwa kiasi gani mtoto wake kwani bado hajawa na uelewa wa kupambanua mambo ingawa kwa upande wake imemuathiri
Roma amesema kuwa kwa tukio lililotokea wapo watoto wadogo wanaoweza kuzungumza lakini kwa mwanae Ivan wamejitahidi kumficha ingawa siku akikua atakutana na picha za majeraha na habari zinazohusu namna watanzania walivyopaza sauti kumuokoa.
"Nilipata matatizo lakini sijui Ivan atakuwa ameathirika kwa kiasi gani kwani sikuonana nae kwa siku nne mfulululizo tangu nilipotoka kwenye matatizo, maana hata nilipokuwa sipo alikuwa akiwaambia watu baba ameenda kufanya show ya viva roma viva, ni mdogo sana siwezi kujua imemuathiri kiasi gani. Ingawa mimi imeniathiri nilihisi napotea na mwanangu bado sijamtengenezea maisha mazuri hii bado inaniumiza akili yangu".
Aidha Roma amesema pamoja na Watanzania kupaza sauti kama njia ya kumkomboa mahali alipokuwa ametekwa na kuteswa japo walionesha upendo lakini waliamua kumlipa deni kwa kupaza sauti kwani hata yeye alijitoa mara nyingi kupaza sauti kwa kusema matatizo yanayoikabili jamii.
"Watanzania mimi siwezi kuacha kuwashukuru hata wakati mwingine nikikaa nafsi yangu inasema nina deni la kulipa, lakini najipa moyo sitaweza kuwalipa fadhila mmoja mmoja ila kwa ninachojaaliwa nitashirikiana nao ingawa ni kama tumeanza upya maisha mimi nilipaza sauti kuhusu matatizo ya jamii kwa takribani miaka 10 tangu wimbo wa kwanza na wao wanakapaza sauti kuniokoa. Nawashukuru sana na ukurasa uliopita tumeshaufunga" Roma aliongeza.