Ni miongoni mwa stori kubwa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii duniani inayohusu shabiki wa kike aliyefanyiwa upasuaji zaidi ya mara 50 ili kuwa na muonekano wa staa wa filamu kutoka hollywood Angelina Jolie.
Sahar Tabar, 22, anatokea Tehran, Iran, amekuwa akiongelewa sana mitandaoni wiki hii, wanaotazama picha hizi kwenye instagram yake wamekuwa na maneno mazuri juu ya kitendo chake huku wengine wakimuita ZOMBIE
Sahar amesema lengo lake kwenye maisha ni kufanana tu na Angelina Jolie na mpaka sasa amepoteza zaidi ya kilo 40 ili kutimiza lengo lake
Tovuti tofauti zinasema ana umri wa miaka 19