Wananchi wa kijiji cha Kyenda kata ya Murukulazo wilayani Ngara mkoani Kagera wameiomba serikali kuchukua hatua juu ya maji yaliyojaa mto ruvubu na kufurika kwenye mashamba yao.
Wakizungumza na Radio Kwizera Kijijini hapo wamesema hali ya mavuno kwa msimu huu ni ngumu kwao baada ya maji kufurika kwenye mto huo na mto Kagera baada ya kuzibwa na mradi wa umeme Rusumo NELSAP.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Ferdinand Festo Masenge amesema mpaka sasa zaidi ya Wananchi 300 wamekwisha athirika na maji hayo ambayo yameharibu kiasi kikubwa cha mazao mashambani.
Naye Diwani wa Kata ya Murukulazo ( CCM ) Bw Mukiza Byamungu amesema mbali na athari za Kilimo lakini pia Sekta ya Afya, Elimu na Biashara zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa baadhi ya walimu, wauuguzi na wanafunzi hutegemea kivuko ambacho kwasasa hakina uwezo wa kutoa huduma.
CREDITS: MWANA WA MAKONDA
Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA |
Saturday, 9 June 2018
HARDNEWZ
No comments:
Post a Comment