• Seynation Updates

    Saturday, 9 June 2018

    Simba yaikalisha tena Yanga SC

    Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, wamewakalisha watani wao wa jadi Yanga SC kwenye majina ya wachezaji walioteuliwa kuwania Tuzo ya mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika wa 2017/18 kwa kuingiza wachezaji sita huku Yanga wakiwa watatu.



    Katika wachezaji hao sita wa wekundu wa Msimbazi wachezaji wanne walikuwemo kwenye kikosi cha Simba msimu huo, huku wawili wakijiunga na klabu hiyo baada ya msimu huo kumalizika.
    Wachezaji hao ni John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya, Erasto Nyoni, Adam Salamba (aliyejiunga na Simba akitokea Lipuli FC) na Marcel Kaheza (Aliyesajiliwa Simba akitokea Majimaji FC) huku Yanga ikiwakilishwa na Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi pamoja na Kelvin Yondani.
    Hayo yamewekwa wazi na Kamati ya tuzo hizo iliyokutana hivi karibuni na ndiyo iliyoteua wachezaji hao 15 miongoni mwa 30 waliotangazwa wiki mbili zilizopita, ambapo pia hao 15 watachujwa kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo na kubakia na wachezaji watatu watakaotangazwa juma lijalo.
     Wachezaji wengine walioingia kwenye orodha hiyo ni pamoja Shafiq Batambuze, Mudathir Yahya na Habib Kiyombo (Singida United), Yahya Zayd na Tafadzwa Kutinyu (Azam), na Hassan Dilunga (Mtibwa Sugar).
    Kwa upande mwingine, Kamati ya Tuzo imesema licha ya Tuzo ya mchezaji bora wa VPL, pia siku hiyo kutatolewa tuzo mbalimbali ikiwemo ya bingwa wa VPL, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji Bora na nyinginezo.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI